Best Kuhusu podcasts we could find (Updated July 2018)
Related podcasts: Katika Education Islamic Religion Msimamo Jihadi Uislam Unafahamu Kiongozi Ikiwa Wafanye Miji Kuishi Kujiripua Mwandamo Makafiri Njia Ibada Maana Majibu  
Kuhusu public [search 0]
show episodes
 
Mada hii inazungumzia msimamo wa Uislam kuhusu kujiripuwa na aina za kujitoa muhanga,hukumu ya kujitoa muhanga,na sababu za kujiripua na uislam wa mwenye kujiripua.
 
Mada hii inazungumzia msimamo wa Uislam kuhusu kuhusu kupigana Jihadi katika njia ya Allah, na upambanuzi wake, na tatizo la waislam wengi kuto fatilia mambo kwa kina, na madhara ya Hamasa.
 
Katika mfululizo wa vipindi vyetu utapata fursa ya kujifunza kuhusu masuala ya uchumi na biashara pamoja na mazingira.
 
Mada hii inazungumzia: Kauli za wanachuoni kuhusu watawala ambao ni makafiri, na hukumu ya Mwanamke kuolewa na mtu wa bid’a.
 
Mada hii inazungumzia hukumu ya kuishi katika miji ya kikafiri na mwongozo kamili kuhusu mambo yanayo takiwa kuyafanya mwislam.
 
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
 
Kupitia vipindi vyetu tunajaribu kuwahamasisha vijana wa Afrika kuhusu elimu ya jamii. Inasaidia kuyafanya maisha yao kuwa rahisi.
 
Mada hii inazungumzia: Daraja za jihadi, ni wakati gani jihadi inakuwa ni lazima, vievile inazungumzia maneno ya wanachuoni kuhusu jihadi.
 
Mada hii inazungumzia ufafanuzi kuhusu maana halisi ya ibada,na mtizamo mbaya ju ya maana ya ibada,na lengo la kuumbwa mwanadamu,na lengo la kutumwa mitume alayhimu ssalam
 
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.Ratiba: Monday-FridaySaa (kwa saa za huku): 06:00UTC saa ya kimataifa 0300Muda: 30Sikiliza: Podcast
 
A
Afisa Afya
Monthly+
 
AfisaAfya ni podcast pekee ya lugha ya Kiswahili itakayokuwa inawaletea mada, mijadala na mahojiano kuhusu afya ya mwanadamu na jinsi ambavyo afya zetu zinaweza kuathiriwa na mazingira tunamoishi, kila siku ya jumapili.
 
M
Mwandamo Wa Mwezi
Daily+
 
Mada hii inazungumzia mwezi mwandamo na uwajibu wa muislam pindi unapo onekana mwezi,na kuwatanabaisha waislam kuhusu ubainifu wa mwezi wa kitaifa na kimataifa,na umuhimu wa kufunga kama alivyo funga mtume (s.a.w)
 
Loading …
show series
 
Ndugu S. Karata akizungumzia Ukaguzi wa Nyama, Majukumu ya AfisaAfya kama mkaguzi wa nyama, sheria zinazosimamia Ukaguzi wa Nyama, malengo ya ukaguzi nakadhalika.
 
Ndugu Swahibu Karata akitoa elimu ya afya kuhusu historia, dalili paka njia za kujikinga na ugonjwa wa homa ya dengi.
 
Historia, visababishi, jinsi unavyoenea, makundi ya watu walio hatarini zaidi, madhara lakini pia ni kwa namna gani tunaweza kujilinda na maambukizi ya ugonjwa wa Listeria - Swahibu A. Karata & Yusuph Uzuwila
 
AfisaAfya Karata akiendelea kujadili chanjo na jinsi ambavyo Chanjo huweza kumkinga binadamu dhidi ya maradhi
 
AfisaAfya Karata akijadili jinsi ambavyo chanjo husaidia kumkinga binadamu na maradhi.
 
Ndugu Swahibu A. Karata akitoa historia yake fupi lakini pia amegusia kidogo kuhusu AfisaAfya podcast
 
Afya kwanza. Bw, Karata akiitambulisha show kwa wasikilizaji wake 😜
 
Afrika ina kiwango kikubwa cha ukataji misitu kuliko mabara mengine yote duniani. Hili lina athari kubwa kwa maisha ya Waafrika kama hawa katika mchezo wetu wanaoishi katika kambi ya wakimbizi baada ya vita vya kikatili.
 
Huku Farahani na Sule wakiota kuwa na maisha bora Ulaya, mwanafunzi Linda tayari yuko njiani kuelekea huko. Mchezo huu unalinganisha ndoto za vijana wa Kiafrika za kusoma na kufanya kazi Ulaya na hali halisi ya mambo.
 
Kila binaadamu hapa duniani ana haki ya uhuru na usawa - kwa mujibu wa azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binaadamu. Lakini katika mataifa mengi barani Afrika, utakuta haki hizi zinaendelea kukanyagwa na kukiukwa.
 
Tatizo linaanzia na ari ya kutaka kumiliki baiskeli mpya ya kifahari. JD hana fedha za kutosha lakini anashindwa kuvumilia na kuchukua mkopo – ingawa hajui atakavyoulipa mkopo huo. Je, somo hili litamuathiri vipi JD?
 
Iwe shuleni, kazini au hata barabarani, familia ya Odhiambo inajikuta ikishinikizwa na athari za ufisadi licha ya juhudi za kutaka kuishi maisha huru yasiyo na dosari ya uovu huu. Watawezaje kuepukana na vitendo hivyo?
 
Hulala kidogo sana, hawafahamu neno „starehe“ lakini wanaipenda kazi yao na wanajitoa kwa jamii wanamoishi. Hili ni jambo linalowaunganisha wafanyabiashara wote wa Kiafrika tunaowatambulisha katika mfululizo wetu mpya.
 
Vipindi vya Noa Bongo vinachunguza kwa kina athari za utandawazi barani Afrika. Kupitia vipindi vyetu wasikilizaji wanaweza kukutana na watu wanaochangia kuufanikisha utandawazi na wale wanaoathiriwa na utandawazi.
 
Katika awamu ya mwisho ya safari, tunaona mabadiliko katika hadithi wakati Tingo anapoonyesha nia ya dhati katika chama. Baki na Zeina wanapatana kwa kinywaji. Tujiunge nao!
 
Tingo hafurahii ufanisi wa chama na huenda akawa na njama fulani. Hii itakuwa na maana gani kwa mashujaa wetu?
 
Hadari amebadili nia na Baki amebadili mipango – hatua inayomfurahisha sana Zeina. Tufuatilie mabadiliko yote yanayoendelea.
 
Katika kipindi hiki Baki anapelekwa hospitalini – nini kilichotokea? Lakini kwanza tutafute jinsi chama kinavyoendelea na vipi mashujaa wetu chipukizi wanavyokabiliana na changamoto.
 
Kwa nini Ben anakataa pendekezo zuri kutoka kwa Tingo, ingawa chama kinahitaji fedha? Kipindi kinapofikia tamati, kitu kingine kinaendelea kati ya Ben na Nana.
 
Mpaka sasa kila kitu kinaonekana kwenda kulingana na mpango. Wanakijiji wanauonaje mradi huo? Tunaungana na mashujaa watatu katika mkutano na Hadari na tusikilize huku wakifanya mkutano wao wa kwanza wa mwaka.
 
Hatua kwa hatua, marafiki zetu wanapiga hatua wanapojaribu na kuungwa mkono na wanakijiji. Hata hivyo uhusiano kati ya Baki na Zeina unaonekana ukichukua mkondo tofauti.
 
Baki, Zeina na Ben wanataka kuanza kwa ufanisi. Kwa bahati mbaya kurejea kijijini huenda kusiwe rahisi kama inavyoonekana na si kila mtu anafurahia kuwaona.
 
Ungana na marafiki zetu wanapofikiria kuvumbua mpango wa biashara kwa chama chao cha kilimo. Lakini Baki ana jambo lengine akilini mwake.
 
Katika vipindi hivi vipya, Ben, Baki na Zeina watatueleza matukio yasiyo ya kawaida wanapoamua kuondoka mjini kwenda kijijini kutimiza ndoto zao.
 
Kwa nini ni muhimu kuwafundisha wavuvi kutumia nyavu ili kuwalinda kaa? Juhudi gani zinaweza kuchukuliwa kuwalinda Papa? Sikiliza na ufahamu zaidi juu ya hilo na mengine.
 
Kipindi hiki kinazungumzia uvuvi wa kutumia baruti unavyoathiri matumbawe ambayo yanahitaji karne kujengeka, lakini yanaweza kuharibiwa kwa sekunde moja tu. Nini kinachowakumba wanyama na mimea ya baharini?
 
Majangwa barani Afrika yamekuwa yakiongezeka. Hii ni kutokana na shughuli za kibinaadamu duniani kwa mfano ongezeko la malisho pamoja na ukataji miti. Je, ni jinsi gani wakulima wanawajibika kwa hali hiyo?
 
Ukataji miti umesababisha madhara makubwa kwa mazingira. Bara la Afrika limepoteza misitu mingi kuliko bara lingine lolote. Fahamu kuhusiana na biashara haramu ya mbao pamoja na madhara yake.
 
Mahitaji ya mafuta, mkaa na gesi bado ni makubwa. Lakini vyanzo vya nishati hii si vya kudumu, kwa hivyo tutapata wapi nishati hii? Tutaangazia nishati nyingine mbadala na inayoweza kutumika tena kama vile upepo na jua.
 
Afrika inategemea kuni kwa ajili ya kupikia lakini mahitaji ya mkaa yameharibu misitu barani humo. Hebu tuangalie njia mbadala kama vile kupika chakula kwa kutumia joto na mwanga wa jua.
 
Gari ni chanzo kikuu cha uchafuzi wa hali ya hewa. Hutoa hewa ya kaboni inayochangia ongezeko la ujoto duniani. Gundua faida za usafiri wa umma pamoja na baiskeli.
 
Shughuli za kibinaadamu huwa na madhara kwa maisha ya wanyamapori. Tunajua athari za biashara haramu ya nyamapori ambayo ni ya kawaida Afrika. Ni viumbe gani ambao wako katika hatari ya kutoweka?
 
Elimu ya wadudu waharibifu inaweza kuongeza mazao yetu lakini ina madhara makubwa kwa mazingira. Tutaona jinsi sumu ya kuua wadudu inavyojipenyeza kwenye ardhi na maji. Tutajifunza jinsi ya kufanya kilimo cha zao moja.
 
Suala la takataka limekuwa ni tatizo sugu. Na kwa serikali za Afrika kulishughulikia suala hilo ni jukumu kubwa. Tutaelezea hatari ya mifuko ya plastiki kwa viumbe wa baharini, jinsi inavyoharibu mazingira ya majini.
 
Bi Kimasi anaeleza motisha wake wa kupigania nishati zinazoweza kutumika tena na tena. Bodi ya kitaifa inafanya mkutano na waandishi wa habari – Je tangazo lao litalifurahisha jopo letu? Tega sikio!
 
Google login Twitter login Classic login