Ushindi public
[search 0]
More
Download the App!
show episodes
 
Artwork
 
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
  continue reading
 
Loading …
show series
 
Wiki hii, ilikuwa ni mwaka mmoja wa vita nchini Sudan, kati ya jeshi la taifa chini ya Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na wanamgambo wa RSF wanaongozwa na Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo. Mwaka mmoja baadaye, vita vimeendelea na kusababisha vifo vya maelfu ya watu, huku wengine Milioni 8.5 wakiyakimbia makaazi yao wakiwemo Milioni 1.8 waliokwenda k…
  continue reading
 
Wiki iliyopita, Somalia ilimfukuza nchini mwake Balozi wa Ethiopia Mukhtar Mohamed kwa madai kuwa nchi hiyo inaingilia mambo yake ya ndani. Mwezi Januari, mzozo wa kidiplomasia ulianza kushuhudiwa nchini humo baada ya Ethiopia kuingia kwenye makubaliano na jimbo la Somaliland, kutafuta njia ya kufika baharini na kujenga kambi ya jeshi kwenye ukanda…
  continue reading
 
Kumbikizi ya miaka 30 tangu mauaji ya kimbari yaliyosababisha vifo vya watu hadi laki 8 ,kuna wito wa ulimwengu kuhakikisha watuhumiwa zaidi kusakwa na mataifa yaweke mikakati kuzuia mauaji kama haya kutojirudia Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Human Rights Watch, sasa linataka jumuiya ya kimataifa kuongeza kasi ya kuwasaka watuhum…
  continue reading
 
Bassirou Diomaye Faye amechaguliwa kuwa rais mpya wa Senegal. Faye mwenye umri wa miaka 44, mshirika wa karibu wa mwanasiasa mwenye ushawishi Ousamane Sonko, ameahidi kufungua ukura mpya wa uongozi wa nchi hiyo. Kwanini raia wa Senegal wamemchagua Faye ? Tunachambua pamoja na Mali Ali akiwa jijini Paris, na Lutege Musa Lutege akiwa jijini Dar es sa…
  continue reading
 
Nchini Burundi, chama kikuu cha upinzani cha CNL kinashuhudia mgawanyiko baada ya kiongozi wake Agathon Rwasa kuondolewa kwenye nafasi kiongozi wa chama. Hii ilitokea wakati Rwasa akiwa ziarani nchini Kenya. Nini hatima ya kisiasa ya Rwasa ? Tunazungumza naye lakini pia Mali Ali mchambuzi wa siasa za Burundi akiwa jijini Paris.…
  continue reading
 
Serikali ya Kenya na Haiti zimetiliana saini ili kufanikisha Kenya kutuma polisi wake nchini Haiti kudhibiti magenge ya wahalifu ambayo yameendelea kutatiza usalama nchini Haiti. Katika makala haya Domic Wabala mchambuzi wa usalama na dkt Braine Wanyama, mchambuzi wa siasa za kimataifa wanatathimini nini maana ya Kenya kutuma polisi kule Haiti.…
  continue reading
 
Viongozi wa Africa wamekutana mwisho wa juma katika mkutano wao wa kila mwaka wa 37, nchini Ethiopia walishindwa kuja na njia ya mapoja kumaliza migogoro barani. Je tatizo la Africa nini? Je Africa inaweza jitegemea? ndio baadhi ya maswali Benson Wakoli, na wachmbuzi mwanadiplomasia Macharia Munene pamoja na mchambuzi wa siasa za kimataifa dkt Brai…
  continue reading
 
Wiki iliyopita, wabunge nchini Tanzania, walipitisha miswada mitatu ya sheria ya uchaguzi kuelekea uchaguzi mkuu mwaka ujao. Tume ya uchaguzi itabadilishwa jina na sasa itafahamika kama Tume huru ya taifa ya Uchaguzi. Mwenyekiti wa Tume na Makamu wake, watateuliwa na rais baada ya kupokea majina matatu kutoka kwenye Kamati ya usaili.Chama kikuu cha…
  continue reading
 
Mataifa ya Mali, Niger na Burkina Faso, yametangaza kujiondoa kwenye muungano wa ECOWAS, baada ya vikwazo ambayo muungano huu ulitangaza dhidi ya mataifa hayo, kipindi baada ya mapinduzi ya kijeshi. Benson Wakoli pamoja na wachanganuzi wa siasa za kimataifa, dkt Braine Wanyama na Mali Ali, wanatathimini Athari ya Niger, Mali na Burkina Faso kujiond…
  continue reading
 
Wimbi la siasa imeangazia fursa iliyopo kidiplomasia kwa rais wa DRC Felix Thisekedi aliyeapishwa Jumamosi iliyopita, kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa pili.DR Congo, imekuwa kwenye mvutano wa kidiplomasia na Rwanda, kwa madai kuwa Kigali inawaunga mkono waasi wa M23 eneo la mashariki. Ruben Lukumbuka amewaalika Francois Alwende, mtaalamu wa siasa z…
  continue reading
 
Makala hii imejadili hatua ya rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud kusaini sheria ya kufuta makubaliano kati ya Ethiopia na eneo lililojitenga la Somaliland, hii ikiashiria kutoridhishwa na matumizi ya bandari ya Berbera, uamuzi unaoibua hofu ya kutokea mgogoro baina ya pande hizo mbili.Mwandishi wetu Ruben Lukumbuka ameangazia hili pamoja na mch…
  continue reading
 
Mwishoni mwa wiki jana mjadala umeibuka kati ya wadau wa kisiasa nchini Tanzania kuhusu nini kingekuwa cha kwanza kuwasilishwa bungeni, muswada wa marekebisho ya katiba au sheria za uchaguzi. Ni mjadala ambao umewagawa hata wapinzani, ambapo chama kikuu cha upinzani Chadema chenyewe kinataka katiba mpya kwanza, huku vyama vingine vyenyewe vikisema …
  continue reading
 
Katika makala wimbi la siasa tunaangazia hisia mseto zinazoenea kwenye eneo la ukanda wa nchi za maziwa makuu, baada ya mwishoni mwa juma lililopita, wakuu wa nchi kutoka Jumuiya ya SADC waliokutana mjini Luanda, Angola, kushindwa kutoa terehe kamili ya vikosi vyake kupelekwa mashariki mwa DRC. Aidha, viongozi wa SADC walikubaliana kumpa muda zaidi…
  continue reading
 
Siku chache baada ya rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi kutangaza kulegeza hatua kwa hatua makataa ya hali ya dharura kwenye majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri mashariki mwa nchi hiyo, wiki hii bunge la seneta lilikutana na kuongeza muda wa hali hiyo, Ungana na mwandishi wetu Victor Moturi pamoja na Omari Kavota mtaalamu wa s…
  continue reading
 
Mataifa mbalimbali dunia, yamelaani hatua ya kundi la Hamas kutoka Mamlaka ya Palestina kushambulia miji mitatu ya Kusini mwa Israeli na kurusha maelfu ya maroketi kutokea ukanda wa Gaza. Aidha Urusi imesema kuundwa kwa taifa la Palestina, ndilo suluhu kwa mzozo wa Isreali na Palestina, waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov, akisema vita ha…
  continue reading
 
Loading …

Quick Reference Guide