Iniaes public
[search 0]
More
Download the App!
show episodes
 
Loading …
show series
 
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres asubuhi ya leo saa za New York, Marekani kupitia Hotuba Maalumu kuhusu Hatua Dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi ametahadharisha kuhusu hatari ya wazi ya uwezekano wa ongezeko la joto juu ya nyuzijoto 1.5 za selsiasi linaloukabili ulimwengu ikiwa uzalishalishaji wa hewa chafuzi utaendelea kwa viwango vy…
  continue reading
 
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hususan mashariki mwa taifa hilo la Maziwa Makuu, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, MONUSCO umeanzisha mfumo wa kutoa tahadhari mapema kuhusu mashambulizi dhidi ya raia yanayoendeshwa na waasi kwenye mji wa Bunia jimboni Ituri. Mfumo huu unaweza jamii, jeshi la serikali na MONUSCO kubadilisha…
  continue reading
 
Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Usalama wa Chakula, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO limeripoti kwamba kila siku, takribani watu milioni 1.6 kote duniani huugua kwa kula chakula kisicho salama na karibu asilimia 40 ya mzigo huo ukibebwa na watoto wadogo, chini ya umri wa miaka mitano. Hii leo kupitia mkutano wa pamoja wa waandi…
  continue reading
 
Hii leo jaridani tunaangazia usalama wa chakula, na ripoti ya ILO kuhusu suala la ajira Gaza wakati huu wa machafuko. Makala tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na mashinani tunakupeleka nchini Sudan, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Usalama wa Chakula, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO limeripoti k…
  continue reading
 
Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO inaweka bayana ni kwa vipi vita iliyoanza tarehe 7 Oktoba mwaka jana wa 2023 inasukuma kiwango cha ukosefu wa ajira kufikia takribani asilimia 80 huku pato la ndani la ukanda wa Gaza likipungua kwa asilimia 83.5. Takwimu hizo zinamaanisha kuwa kati ya kila watu 10 Ukand…
  continue reading
 
Katika Jarida la habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea -Gaza Nuiserat Israel imeshambulia shule moja iliyokuwa inahifadhi wakimbizi 6,000 wa kipalestina na kuua watu 35, na wengine wengi wamejeruhiwa,-Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa leo kumefanyika tukio la kukumbuka wafanyakazi 188 wa chombo hicho waliouawa mwaka 2023 pek…
  continue reading
 
Leo ni siku ya mazingira duniani na Umoja wa Mataifa unaisa dunia kuchukua hatua sasa kurejesha Uhai wa ardhi iliyoharibiwa na kujenga mnepo dhidi ya kuongezeka kwa hali ya jangwa na ukame na hiyo ndio kaulimbiu ya siku ya mwaka huu. Akisisitiza maudhui hayo Inger Andersen Mkurugenzi mtendaji wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP amemtak…
  continue reading
 
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya mazingira duniani, na msaada wa kibinadamu nchini Haiti. Makala tunamulika hatua za kurejesha afya ya ardhi iliyoharibiwa na mashinani tunasalia hapa makao makuu kusikia ujumbe wa Martin Griffiths anayestaafu mwishoni mwa Juni. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres asubuhi ya leo saa za New York, Mare…
  continue reading
 
Licha ya machafuko na mashambulizi yanayofanywa na makundi yenye silaha huko nchini Haiti, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani limeendelea kuimarisha operesheni zake katika mji mkuu wa Port-au-Prince na kusaidia jamii zilizoathiriwa na ghasia ambapo kwa mwezi Mei shirika hilo limeweza kuwafikia zaidi ya watu 93,000. Kwa mujibu …
  continue reading
 
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya ambako UNICEF na wadau wake imefanikisha utengenezaji wa sodo za kufuliwa. Piatunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za Gaza, wahamiaji kutoka bara la Afrika na watoto katika migogoro. Mashinani inatupeleka nchini DR Congo, kulikoni?Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala…
  continue reading
 
Baiskeli! Umoja wa Mataifa uliitambua rasmi umuhimu wake tarehe 13 mwezi Machi mwaka 2022 kwa kupitisha azimio la kutambua tarehe 3 mwezi Juni kila mwaka kuwa siku ya baiskeli duniani. Umuhimu wake kama chombo cha usafiri chenye gharama nafuu, hakichafui mazingira na zaidi ya yote afya kwa watumiaji kwani ni mazoezi. Huko Nairobi, mji mkuu wa Kenya…
  continue reading
 
Watu milioni moja sasa wamefungasha virago na kuukimbia mji wa Rafah kusini mwa Gaza, ka mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, huku kukiwa na ripoti mpya za mashambulizi ya usiku kuamkia leo katika maeneo ya kusini, kati na kaskazini yanayofanywa na vikosi vya Israel. Katika tarifa yake iliyotolewa leo …
  continue reading
 
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na afya ya uzazi nchini Randa. Mashinani tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Watu milioni moja sasa wamefungasha virago na kuukimbia mji wa Rafah kusini mwa Gaza, ka mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, …
  continue reading
 
Nchini Rwanda, hivi karibuni Wizara ya Afya ya nchi hiyo, kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), imeanza usambazaji wa Vidonge vyenye virutubisho vingi vya lishe (MMS) ili kuboresha lishe ya wajawazito kama njia ya kupunguza kasi ya udumavu kwa watoto. Nshimiyimana Clementine, ni Mkuu wa Kituo cha Afya cha Kabaya, Wilayan…
  continue reading
 
Kila uchao, mikutano ifanyika kona mbali mbali za dunia kubonga bongo ni kwa vipi akili mnemba inaweza kutumika kwa manufaa ya binadamu na si vinginevyo kwani Umoja wa Mataifa unataka nyenzo hiyo iwe ya manufaa hasa katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu. Huko Geneva, Uswisi kumetamatika mkutano wa kujadili ni kwa vipi akili mnemba italet…
  continue reading
 
Nchini Kenya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kupitia mradi unofahamika kama GIGA, kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu, wameunganisha wanafunzi zaidi ya 257,000 kwenye mtandao wa Intaneti, wakiwemo wanafunzi 7,690 wenye mahitaji maalum, na pia mafunzo ya kidijitali kwa maelfu ya walimu.Mmoja wa walimu walionufaika na mafunzo …
  continue reading
 
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Burkina Fasso na mradi unofahamika kama GIGA unaosaidia kufanikisha masomo ya kidijitali kwa wanafunzi nchini Kenya. Makala inamulika usimamizi wa Akili Mnemba na mashinani inatupeleka Garissa nchini Kenya, kulikoni?Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo ameelezea wasiwas…
  continue reading
 
Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo ameelezea wasiwasi mkubwa kufuatia ongezeko la hivi karibuni la mauaji ya raia nchini Burkina Faso, huku kukiwa na madai pande zote, makundi yenye silaha na serikali kuhusika na mauaji hayo. Kwa mujibu wa tarifa ya ofisi ya Kamishina Mkuu wa haki za binadamu OHCHR kati ya Novemb…
  continue reading
 
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika ni kwa vipi wabunifu wanaweza kumiliki kazi zao na zikasongesha SDGs ikiwemo kutokomeza umaskini. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za Sudan, Gaza na jukwaa la Kimataifa la “AI for Good”, pamoja na uchambuzi wa neno la wiki.Mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa leo yametoa onyo kali k…
  continue reading
 
Makala hii inatupeleka nchini Sudan kuangazia maisha ya Sara, mmoja wa wakimbizi wa ndani katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika. Sara alikuwa na ujauzito wa miezi 9 wakati bomu lilipopiga nyumba yake na kumlazimu kukimbia na hatimaye kujifungua mtoto wake peke yake bila uangalizi wowote wa kitabibu. Familia nyingi nchini Sudan zimesambaratishwa …
  continue reading
 
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya kimataifa ya walindaamani wa Umoja wa Mataifa. Makala inatupeleka nchini Sudan kusikia simulizi ya mmoja wa wakimbizi na mashinani tunakupelekea nchini Ethiopia kusiki jinsi ambavyo wasichana wanavyosaidiwa kubaki shule.Leo ni siku ya kimataifa ya walindaamani wa Umoja wa Mataifa mwaka huu ikibeba maudhui “Kuwa …
  continue reading
 
Leo ni siku ya kimataifa ya walindaamani wa Umoja wa Mataifa mwaka huu ikibeba maudhui “Kuwa tayari kwa ajili ya ujenzi wa mustakbali bora kwa pamoja”. Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa ulinzi wa amani unasialia kuwa ushirikiano wa kipekee wa kimataifa. Katika ujumbe wake kwa siku hii Antonio Guterres amesema "Leo tunawaenzi walinda amani zaidi ya …
  continue reading
 
Mshauri wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kijeshi, Jenerali Birame Diop amesema kadri binadamu wataendelea kuweko duniani mizozo na majanga yataendelea kuweko na hivyo kinachohitajika ni mfumo wa kupunguza uweko na utatuzi wa majanga hayo.Akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha siku ya walinda amani duniani, Jenerali Diop amba…
  continue reading
 
Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea-Watu zaidi ya 2000 wahofiwa kufunikwa na maporomoko ya udongo Papua New Guinea , Umoja wa Mataifa wasaidia-Ripoti ya UNRWA inasema wakimbizi wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na dharura ya kiafya isiyokuwa na mfano wake iliyosababishwa na vita mbaya zaidi ka…
  continue reading
 
Mahakama ya kimataifa ya haki ICJ leo imetoa maamuzi ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari katika Ukanda wa Gaza Flora amefuatilia uamuzi huo.Leo Kwa kura 13 dhidi ya 2 mahaka ya ICJ imeamua kwamba:1. Inathibitisha tena hatua za muda zilizoainishwa katika Maagizo ya…
  continue reading
 
Ripoti mpya ya Takwimu za Afya Ulimwenguni iliyotolewa leo na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, inaonyesha kuwa janga la COVID-19 limebadilisha mwelekeo wa kuongezeka kwa umri wa watu kuishi wakati wa kuzaliwa na matarajio ya maisha yenye afya wakati wa kuzaliwa HALE.Ripoti hiyo ya takwimu za afya ulimwenguni hutolewa kila mwaka na W…
  continue reading
 
Zikiwa zimesalia siku chache kufika Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa kila Mei 29, tunaangazia shughuli zao na kuwatia moyo na leo tunaelekea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuwasikia baadhi yao kutoka katika Kikosi cha 7 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mat…
  continue reading
 
Nchini Tanzania, kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) na wadau wake kama Kitovu cha Kuratibu Mifumo ya Chakula cha Umoja wa Mataifa, Kikundi cha Washirika wa Maendeleo ya Kilimo na Lishe, wakulima, sekta binafsi, na watafiti na Taasisi za kitaaluma wamekutana mjini Morogoro ili kupitia na kuboresha vipaumbele na ra…
  continue reading
 
Hii leo jaridani tunaangazia maamuzi ya ICJ ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel, na mifumo ya chakula nchini Tanzania. Makala inatupeleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR na mashinani nchini Kenya, kulikoni? Mahakama ya kimataifa ya haki ICJ leo imetoa maamuzi ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Kuzui…
  continue reading
 
Hii leo jaridani tunakuletea mada ka kina inayotupeleka huko wilaya ya Abyei iliyoko kati ya mpaka wa Sudan Kusini na Sudan lilifanyika shambulizi la kuvizia wakati gari la Umoja wa Mataifa lilipokuwa likisafirisha raia waliojeruhiwa, ambalo lilisababisha kifo cha mlinda amani. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa methali “Kanga haza…
  continue reading
 
Kenya inashuhudia kiwango kikubwa cha mvua zaidi ya kile cha kawaida ambacho kimesababisha mafuriko makubwa,maporomoko ya udongo na maelfu ya watu kutawanywa hivi karibuni. Miongoni mwa maeneo yaliyoathirika zaidi ni Kaunti ya Garisa , ambako hivi sasa asante kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na wadau wake kama shirika la N…
  continue reading
 
Ghasia zikiwa zinaongezeka katika mji mkuu wa Haiti, Port-Au-Prince, hospitali sita kati ya kumi nchini humo ziko katika hali mbaya ya utoaji huduma limeonya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF.Taarifa ya UNICEF iliyotolewa leo mjini Port-Au-Prince imeeleza kwamba vurugu zimeutikisa mfumo wa afya wa Haiti unaoporomoka kutokana n…
  continue reading
 
Hii leo jaridani tunaangazia huduma za afya kwa watoto nchini Haiti na simulizi afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO kuhusu yanayoenndelea Gaza. Makala tnakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni? Ghasia zikiwa zinaongezeka katika mji mkuu wa Haiti, Port-Au-Prince, hospitali sita kati ya kumi nchini humo …
  continue reading
 
Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO aliyerejea hivi karibuni kutoka Ukanda wa Gaza amesimulia yale aliyoshuhudia akiwa huko huku huku akisisitiza kuwa "hakuna mahali salama" katika Ukanda huo na aliyoshuhudia ni “yakusitikisha na ya kutisha.”Ni Nika Alexander kiongozi wa timu ya mawasiliano ya dharura kutoka WHO akieleza to…
  continue reading
 
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kufuatilia mradi wa mradi wa Cookfund, Elisabeth Ngoye amezungumza na Laurien Kiiza wa UNIC Dar es Salaam. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za afya, Gaza na Ukraine. Mashinani inatupeleka nchini Kenya, kulikoni? Ripoti mpya iliyotolewa leo Mei 21 na Shirika la Umoj…
  continue reading
 
Makala hii inamwangazia Meja Lilian Laizer, Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa anayehudumu katika Kikosi cha 7 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR chini ya MINUSCA ambao ni Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini humo. Meja Lilian Laizer anashughulika na masuala ya jinsia na wato…
  continue reading
 
Kuongezeka kwa shughuli za kijeshi huko Rafah, kusini mwa Gaza, kumesababisha mamia kwa maelfu ya watu kuyahama makazi yao, na kufanya maisha kuwa magumu zaidi kwa maelfu ya familia ambazo tayari zimelazimika kuyahama makazi yao mara kadhaa. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP lina wasiwasi mkubwa kwamba hali hii ya kuhama …
  continue reading
 
Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya sheria na uhalifu na hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza. Makala tunakupeleka nchini CAR kufatilia kazi za walinda amani na mashinani tunakuletea ukumbe kuhusu ufugaji nyuki na thamana yao. Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, Karim Khan ametangaza leo Mei 20 maombi ya hati za ku…
  continue reading
 
Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, Karim Khan ametangaza leo Mei 20 maombi ya hati za kukamatwa viongozi wa Hamas na Israel kwa madai ya kuhusika na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika eneo la Gaza. Ni Karim Khan, Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu mapema leo alipotangaza kwamba ana…
  continue reading
 
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) leo limetoa Orodha mpya ya inayojumuisha familia 15 za bakteria zenye usugu dhidi ya viuavijiumbe maradhi au antibiotics. Orodha hiyo inatoa mwongozo kuhusu maendeleo ya matibabu mapya na ya lazima ili kukomesha kuenea kwa usugu dhidi ya dawa. Katika taarifa iliyotolewa leo, WHO inafafanua kuwa usug…
  continue reading
 
Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya katikati ya mwaka ya hali na mtazamo wa uchumi wa Dunia kwa mwaka 2024 iliyotolewa leo inaonyesha matarajio ya kiuchumi duniani yameboreka tangu utabiri uliotolewa Januari 2024, lakini mtazamo ni wa matumaini yanayohitaji tahadhari. Je, Afrika hali iko vipi? Flora Nducha amezungumza na Nelly Rita Muriuki mchumi kutoka …
  continue reading
 
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya usugu dhidi ya viuavijiumbe maradhi au antibiotics, na hali ya kibinadamu nchini Ukraine. Makala tunasalia hapa hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa na mashinani tunaelekea nchini Afghanistan, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) leo limetoa Orodha mpya ya inayojumuisha familia 15 za bakt…
  continue reading
 
Mashirika ya kibinadamu yanafanya kazi bila kuchoka kusaidia kuwaondoka raia katika eneo la Kharkiv ambalo siku za hivi karibuni limeshuhudia kuzorota kwa hali ya usalama na kutanda kwa wimbi la mapigano ambayo yamesababisha vifo vya raia na majeruhi ikiwa ni pamoja na watoto. Video ya ofisi kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura ya U…
  continue reading
 
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Bahrain kwenye mji mkuu Manama, ambako wajasiriamali wamekusanyika kwa lengo la kutumia ugunduzi na ujasirimali kusongesha SDGs. Pia tunakuletea muhtasariwa habari kutoka ICJ, WHO na huko huko Bahrain, pamoja na uchambuzi wa neno “HIZAYA.”Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterre…
  continue reading
 
Huko Manama mji mkuu wa Bahrain huko Asia ya Magharibi kunafanyika mkutano wa tano wa Jukwaa la Uwekezaji kwa wajasiriamali, WEIF 2024. Zaidi ya washiriki 1000 ni wajasiriamali kutoka Afrika wakisaka kujenga mitandao na ubia ili kusaka masoko ya uhakika ya bidhaa zao na hatimaye kuondokana na umaskini, moja ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ya…
  continue reading
 
Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Catriona Laing ameendelea na ziara yake ya kuwaaga viongozi wa eneo hilo na sasa ametembelea Somaliland. Juzi Mei 12, Catriona Laing alikuwa Dusmareb, mji mkuu wa jimbo la Galmudug katikati mwa Somalia ambako alipongeza juhudi za kupambana na ukeketaji. Kisha jana Mei 14 akatua Har…
  continue reading
 
Loading …

Quick Reference Guide